Alhamisi , 9th Nov , 2023

Wananchi wa vijiji Lualaje na Mwiji kata Lualaje Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya wameiomba Serikali kuharakisha ujenzi wa daraja la Lualaje linalounganisha kata hiyo na Mapogolo Wilaya ya chunya kabla ya msimu mvua kuanza ili kuwarisihia usafarishaji wa pembejeo na mazao kutoka mashambani.

Baadhi ya Watendaji wa Serikali na Maafisa wengine wakiwa wameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Homera kwenye ziara yake Kata ya Lualaje.

Akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa Juma Homera aliyefanya ziara katika kata Lualaje Yusuph Mwangoka mkazi wa kijiji cha Lualaje  amesema wanaishukuru Serikali kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi daraja  hilo na kwanj likikamilika  litapunguza gharama za maisha na adha ya usafiri nanusafirishaji wa mazao,pembejeo na abiria. 

Mwangoka amesema kuwa kwa sasa wanatumia gharama kubwa kusafirisha mazao ya mashambani kama vile Tumbaku, pembejeo za kilimo na  bidhaa za madukani hivyo wanaiomba Serikali kuharakisha ujenzi wa daraja hilo ili kupunguza gharama za uzalishaji. 

'Kama ulivyoona kata yetu wananchi wanashughulika kilimo hivyo ujenzi  wa daraja hili ambalo linaunganisha kata Lualage na Kata ya Mapogolo hivyo kukamilka kutapunguza gharama za uzalishaji hivyo kumpa nafuu mwananchi wa kawaida cha msingi tunaomba likamilishwe kwa wakati kabla ya mvua hazijaanza" anasema Mwangoka

Mwangoka anasemema wananchi katika kata hizo wanashughulisha na kilimo cha tumbako na mtumba mmoja wa tumbako wanasafrishi kwa shilingi 5000/= lakini daraja likikamika gharama zitapungua hadi kufikia shilingo 1400/= kutoka shambani kwenda kwenye maghala hivyo wanaiomba serikali imlipe mkandarasi haraka ili aweze kukamilsha ujenzi wa daraja hilo.

Akisoma taarifa ya ujenzi wa Daraja hilo Meneja wa TARURA Wilaya Chunya Mhandishi Emmanuel Kayola amesema gharama za mradi ni milioni 210 ujenzi wake umefikia asilimia 75 na mpaka sasa mkandarasi hajalipwa na anaendelea na ujenzi na matarajio ifikapo Disemba mwaka huu ujenzi uweumekamilika. 

Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera amemtaka Mkandarasi kufanya haraka Ukamilishwaji wa Daraja hilo ambalo ni tumaini kwa Wasafrisha Mazao na Wanafunzi ambao wanategemea Daraja hilo kuvuka Kuwahi Masomo Shuleni.

"Kama unavyofahamu Maji yakijaa pale hakuna mwanafunzi wala mtoto atakayepita hapo kwa hiyo naomba Uongozi wa Kijiji na Kata mbali na Mkandarasi kufanya haraka ukamilishwaji wa daraja hili lakini pia nyie msaidieni mkandarasi vifaa vyake visiibiwe." amesema Juma Homela Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.