Ijumaa , 15th Apr , 2022

Jeshi la Uhamiaji Mkoa wa Dodoma linamshikilia mtanzania Tito Mbwilo (43) mkazi wa Iringa kwa tuhuma za kusafirisha wahamiaji haramu watano raia wa Ethiopia 

Akiongea na waandishi wa Habari Afisa uhamiaji Mkoa wa Dodoma Bahati Mwaifuge amesema  wahamiaji hao haramu walikamatwa April 3 mwaka huu katika kijiji cha Mtera wakielekea Tunduma Mkoa wa Songwe

."Jeshi letu la uhamiaji tumefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu watano akiwemo mtanzania mmoja wakisafirishwa kwenye gari yenye namba za usajiri T991 DXB Toyota Rumioni ambalo lilikuwa linaendeshwa na Tito Mbwilo akijua ni kosa"