Wakizungumza katika mkutano uliohusisha wafugaji na uongozi wa serikali ya wilaya ya Morogoro wafugaji hao wamesema wameridhika na maelezo yaliyotolewa na serikali kuhusu kuchukua hatua dhidi ya madereva wa bodaboda waliokuwa wakiwavamia wafugaji.
Pia wamesema wanataka kuona hatua sahihi zikichukuliwa na kuona fidia zinatolewa kwa wafugaji walioathirika katika migogoro hiyo.
Naye mkuu wa wilaya ya Morogoro Saidi Amanzi amesema atafikisha malalamiko ya wafugaji katika ngazi za juu lakini pia amewakumbusha kuanza kufikiria kupunguza mifugo na kuanza kuwekeza.
Mkuu wa polisi wa wilaya Zuberi Chembela amewatoa hofu wafugaji waendelee kufanya shughuli zao za maendeleo mjini Morogoro na kueleza hatua walizozichukua kwa madereva wa boda boda waliobainika kuwapiga wafugaji mjini Morogoro.
Nje ya mkutano wafugaji wamesema sasa imetosha kwa migogoro ya wakulima na wafugaji na kuomba dola kusimamia sheria za ardhi zilizopo kwa kuheshimu mipaka ya kisheria katika vijiji vilivyotengwa kwa ajili ya wakulima na wafugaji ili kuondoa muingiliano wa shughuli za kilimo na ufugaji