
Mbunge wa jimbo la Kiteto, wakili msomi Edward Kisau Ole Lekaita
Mbunge wa jimbo la Kiteto, wakili msomi Edward Kisau Ole Lekaita, amesema majosho hayo yatajengwa katika vijiji vya Makame, Mwitikira, Loolera, Katikati na Ngabolo.
"Lengo ni kwa ajili ya kuboresha afya za mifugo na tumepatiwa sh80 milioni fedha hizo kutokana na ziara ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega aliyoifanya mwanzoni mwa mwaka huu mifugo ilipokufa kwa ukame," amesema Ole Lekaita,
Amesema fedha walizopata ni za ujenzi wa josho la kijiji cha Loolera kata ya Loolera shilingi milioni 16, josho la kijiji cha Mwitikira kata ya Kiperesa shilingi milioni 16 na josho la kijiji cha Katikati kata ya Makame shilingi milioni 16.
Amesema ujenzi wa josho kijiji cha Ngabolo kata ya Ndedo ni shilingi milioni 16, na josho la kijiji cha Makame kata ya Makame shilingi milioni 16.
"Kwa niaba ya wananchi wa jimbo la Kiteto, tunamshukuru sana Rais mama yetu mpendwa Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake wote Serikalini kwa kugusa maisha yetu wana Kiteto," amesema Ole Lekaita.
Amesema majosho hayo yatasaidia kuboresha sekta ya mifugo kama ilivyoelekezwa kwenye ilani ya CCM 2020-2025 ya kujenga Majosho katika Vijiji vyenye mifugo.