
Meneja kituo kikuu cha mabasi Ubungo Maira Mkama
Akizungumza na kurasa hii leo Meneja huyo amesema tayari serikali imetangaza kutafuta mzabuni na kwamba baada ya kupatikana taratibu zingine zitafuata kwa wafanyabiashara watakaokidhi vigezo vilivyowekwa ili wapewe maeneo ya kufanyabiashara zao kwenye kituo hicho.
Meneja huyo ameongeza kuwa kila mwananchi ana haki ya kufanya biashara katika eneo hilo ambapo amewatoa hofu wafanyabiashara hao na kudai kuwa hakuna mgogoro wowote utakaotokea kutokana na utaratibu mzuri uliowekwa ili kugawa maeneo ya kufanyiabiashara katika eneo hilo.