Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania, Johnson Minja akiwa Mahakamani.
Wito huo umetolewa jana na Minja wakati akifungua kikao cha Halamshauri Kuu ya Taifa ya Jumuiya hiyo kilichofanyika mjini hapa ambapo alisema tayari viongozi wa ngazi za juu wa Jumuiya hiyo wameshawasili kuhudhuria kesi hiyo.
“Ni siku moja tu kabla ya siku ya kesi ambayo imefunguliwa Dodoma, jumuiya ya wafanyabiashara wanahudhuria kesi kwa pamoja kama taifa,” alisema Minja na kuongeza kuwa.
“Lakini pia, kumekuwa na muunganiko wa watu wengi ambao wanataka kujua maendeleo ya kesi na kitu gani kinaendelea, naomba wafanyabiashara wawe na amani na utulivu wakati kesi hiyo ikiwa inaendelea.”
Amesema tunaamini kwamba mahakama itatenda haki na mwisho wa siku yale ambayo tumejadiliana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Serikali kwa ujumla, yanaweza kufanyiwa kazi kwa aajili ya manufaa na maslahi mapana zaidi ya Taifa , wafanyabiashara na wananchi wote kwa ujumla.
Amesema, haitakuwa na maana kama viongozi wote watakuwa mahakamani na wafanyabiashara nao wakafunga maduka yao hali itakayosababisha wao na Serikali kukosa mapato na wananchi kukosa huduma.
“Haina maana sisi tuna kesi na wao waendelee kupoteza wanapofunga maduka yao, wao wanapoteza ,wananchi wanakosa huduma na Serikali inakosa mapato, kikubwa tunachoomba kwao ni sala, watuombee lakini wasisitishe huduma, ili watoe huduma kwa wananchi na Serikali ipate mapato,” alisema Minja
Vile vile amesema, kitendo cha wafanaybiashara kufunga maduka yao yao wakati kesi hiyo ikiendelea mahakamani,inaweza kusababisha Jumuiya hiyo kushindwa kufikia azma yao kwa Serikali ya mazungumzo katika kuwasaidia kufikia muafaka wa changamoto zinazowakabili , kwa njia ya majadiliano.
Leo Minja anatarajiwa kufikishwa mahakamani kwa mara ya pili, mara ya kwanza alifikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma mjini mnamo Januari 28 mwaka huu kwa tuhuma ya kuwachochea wafanyabiashara wasilipe kodi ya Serikali.
Pia Minja anatuhumiwa kwa kosa la kuwapa maelekezo wafanyabiashara ya kutotumia mashine za Kilektoniki (EFDs).