Alhamisi , 30th Jul , 2015

Jumuiya ya wafanyabiashara hapa nchini imesema kuwa itahakikisha kuwa inakaa na wagombea wa urais hapa nchini ili kutaka kujua kama atawasaidia ili wamuingize madarakani na kumjazisha mkataba kwa ajili ya kumfuatilia kama atatekeleza waliyo kubaliana

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabaisahra nchini Tanzania Johnson Minja akizungumza na Wafanyabiashara pamoja na Waandishi wa Habari hawapo Pichani

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufungua ofisi ya jumuiya ya wafanyajiashara mkoani Njombe mwenyeki wa jumuiya hiyo taifa Jonson Minja jana amesema kuwa watawakalisha wagombea wa urais ili kujua atawafanyia nini na ili wamchague kuwa rais.

Minja Amesema kuwa mkutano huo utakao jumuisha wafanyabiashara wote nchini utafanyika jijini Dar Es Salaam, na kuwashirikisha wagombea wote ili wajue atafanyiwa nini baada ya kuingia madarakani.

Amesema kuwa baada ya mkutano huo na wagombe wa urais watawajazisha mkataba wa makubaliano yao na watafuatilia kwa makini kile walichokubaliana nae ili kuinua uchumi wa wafanyabiashara na nchi kwa Ujumla.

Katika hatua Nyingine Minja amesema kuwa wanapenda kulipa kodi na wanawahimiza wafanyabishara kwenda kulipa kodi kwa kuwa suala la kodi ya ongezeko kwa asilinia 100 wamelishughulikia na sasa ni asilimia 50 na kuwa wamefikia muafaka wa kuwa kodi itatakiwa kupanda kulingana na ongezeko la uchumi.

Ameongeza kuwa kuhusu suala la mashine za kutolea risiti za kielekroniki EFD zilizo leta mgogoro, Serikali kwa kushirikiana na wafanyabiashara wanaendelea na mchakato wa kujifunza katika nchi za jirani huku akisema wameenda Uganda na kuna nchini nyingine wanatarajia kwenda.