
Katika mkutano uliofanyika kwa njia ya mtandao na kuwashirikisha wafanyabiashara hao miongoni mwa wachangiaji ni mfanyabiashara Azim Dewji ambapo amesema kuimarika kwa Bandari ya Dar es salaam kutasaidia mataifa tegemezi ya bandari hiyo
"Watanzania waelewe kwamba hii Bandari sio ya watanzania pekee Tanzania tunaimiliki ila inasaidia nchi saba, kwahiyo kuna biashara kubwa sana ambayo inaweza ikafanyika"
Katika mkutano huo pia ameshiriki Mkurugenzi wa Mipango wa TPA Dr. Boniphace Nobeji ambapo amesema serikali ya Tanzania imeendelea kuwa na uwekezaji mkubwa kwenye bandari huku akisema uwekezaji huo umekuwa na manufaa
"Hadi kufikia Juni 2022 tulihudumia jumla ya shehena milioni 20.5 kwa ujumla, na kati ya hizo zilihudumiwa katika bandari ya Dar es salaam ni milioni 18"
"Kwa mantiki hiyo kuna haja ya kuboresha huduma za kibandari kwa ujumla wake, na serikali kwa miaka yote imeendelea kuwekeza kuhakikisha inaboresha huduma hizi"
Aidha mwenyekiti wa wamiliki wa Malori Tanzania Chuki Shabani amesema maboresho ya bandari ya Dar es salaam yaende sambamba na uwekezaji kwenye barabara ili kuondoa kero wanazokutana nazo katika kusafirisha mizigo
"Suala la bandari kwetu sisi ni la muhimu sana, kwa sababu bila mizigo hatuwezi kufanya biashara ipasavyo, ukisikia kuna nchi nane ambao ni wadau wa bandari yetu, karibu asilimia 70 au 80 wanategemea kusafirisha mizigo kupitia malori yetu"
"Pale inapotokea uwekezaji ambao una tija kwetu sisi ni muhimu zaidi, tungependa sana uwekezaji wa bandari utizame bandari kwa upana wake pamoja na barabara zake"
"Sisi kama wasafirishaji tunaomba sana ubora wa bandari ili tuweze kupata mizigo, lakini isiwe bandari peke yake ile sehemu ya maji, iangaliwe pia hiyo mizigo itafikaje inakokwenda?"
Naye Mwenyekiti wa Chama cha waendesha bandari kavu Meleck Shange amesema uwekezaji kwenye bandari hiyo utasaidia kuongeza wingi wa bandari kavu nchini kwani kwa sasa zipo 14
"Ukiangalia uwekezaji ambao unafanyika sasa bandarini tunategemea hata namba ya bandari kavu ambazo tunazo utaongezeka"
"Kwa sasa tuna bandari kavu 14 za makasha, ambayo ni makasha yenye mizigo sio matupu, na bado nyingi zinazidiwa na mzigo, tunaamini jinsi muwekezaji atavutia meli nyingi kuja Dar es salaam sisi pia tutapata kazi kubwa zaidi"