Alhamisi , 7th Jul , 2016

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Luhaga Mpina amesema serikali kupitia wizara hiyo wametoa muongozo kwa halmashauri zote nchini kuanza kuwakamata wachafuzi wa mazingira na kuwatoza fini kuanzia laki mbili na kuendelea.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Luhaga Mpina amesema serikali kupitia wizara hiyo wametoa muongozo kwa halmashauri zote nchini kuanza kuwakamata wachafuzi wa mazingira na kuwatoza fini kuanzia laki mbili na kuendelea sambamba na kuwafunga jela kwa miezi isiyopungua sita.

Naibu Mpina ameyasema hayo kwenye mahojiano maalumu na East Africa Radio na kuongeza kuwa kila mtanzania anapaswa kuzingatia usalama wa mazingira wa eneo lake kulingana na taratibu na kanuni zilizopo sambamba na miongozo iliyowekwa.

Sambamba na hilo amewataka wafanyabiashara walioingia mikataba yakuzoa taka na halmashauri mbalimbali nchini wafanye shughuli hiyo kikamilifu ili kuzuia takataka hizo zisizalishe magonjwa.

Amezitaka mamlaka husika zifanye kazi za kutunza mazingira sambamba na kutokuwa na upendeleo wowote katika kutoa adhabu kwakuwa kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi kuwepo kwa upendeleo wa adhabu zinazotolewa kuwa na ubaguzi.