Mambosasa ametoa kauli hiyo jijini Dar es salaam sema wananchi hao walikuwa wakielekea Ubalozi wa Afrika Kusini, kwa ajili ya kushinikiza kuachiwa kwa ndege ambayo inashikiliwa na Serikali ya Afrika Kusini kwa amri ya Mahakama.
"Kwanza sisi Jeshi la Polisi haturuhusu maandamano, na pia hatuhusu mtukufanya anavyojisikia yeye baada ya kupata aarifa nilimwagiza RPC ilala ili kuchukua hatua za kuzia maandamanpo pili kuwakamaa waratibu wa maandamano."
"Chochote ambacho wanataka kupelekea kwa umma wanaweza kuandika, wanweza kutuma Mwakilishi" amesema Mambosasa.
Kwa sasa nchini Afrika Kusini kuna ndege ambayo ni mali ya Tanzania inashikiliwa kutokana na kuwepo kwa kesi ya muda mrefu iliyomuhusisha mkulima mmoja ambaye alikuwa akiishi Tanzania kufuatia kutaifishwa kwa mali zake alipokuwa akiishi Tanzania.


