Ijumaa , 13th Jun , 2014

Utafiti uliofanywa na Wizara ya Maji na Umwagiliaji nchini Tanzania kuhusu uchunguzi wa vyanzo vya maji umebaini kuwa asilimia 32 ya vyanzo vyote nchini havijaendelezwa kwa kuvuna maji.

Waziri wa maji na umwagiliaji nchini Tanzania Profesa Jumanne Maghembe.

Hayo yamesemwa na Mshauri mwandamizi shirika la maendeleo kutoka uholanzi Frederick Mpendazoe ambapo amebainisha kuwa ni asilimia 68 tu ya vyanzo vya maji nchini ndivyo vinavyofanya kazi.

Hata hivyo mpendazoe amesema kwa sasa kwa kushirikiana na Benki ya dunia wamekuja na uvumbuzi ambao utasaidia katika kuboresha ukusanyaji wa taarifa kuhusu vyanzo vya maji na kupeleka taarifa kwa wahusika ili kuweza kufanya ufuatiliaji.