Jumatatu , 6th Jul , 2015

Bodi za vyama vya msingi vya ushirika wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro zimetakiwa kupitia kwa kina mikataba ya wawekezaji wa mashamba makubwa ya kahawa ili kubaini kama ina maslahi kwa vyama hivyo na serikali.

Mkuu wa Wilaya ya Hai, Anthony Mtaka

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Hai, Anthony Mtaka wakati wa kikao chake na wajumbe wa bodi wa vyama hivyo, wawekezaji, asasi za kifedha, na maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA ili kujadili sekta ya kilimo na utumiaji fursa zilizopo.

Mtaka amesema amefanya Zaira kwa vyama vya msingi vya wilaya hiyo na kubaini kuna changamto kadhaa ikiwemo mfumo wa uendeshaji wa vyama hivyo kuwa mazoea zaidi kuliko kuzingatia utaalamu.

Katika hatua nyingine Mtaka amezitaka taasisi za kifedha kutafisiri kwa vitendo dhana yao ya madirisha ya kilimo na kutoa elimu kwa wakulima namna ya kunafaika na kilimo chao kupitia madirsha yao.