Jumanne , 13th Dec , 2016

Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania imetenga shilingi bilioni tano kama zawadi kwa wateja wake katika msimu huu wa sikukuu za mwisho wa mwaka, kupitia kampeni ijulikanayo kama 'Nogesha Upendo' inayoanza rasmi hii leo.

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Bi. Rosellyn Mworia (Katikati)

 

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Bi. Rosellyn Mworia amesema kila mteja wa Vodacom atapata nafasi ya kushinda pesa taslimu pamoja na nyongeza ya muda wa maongezi na vifurushi vya intaneti kupitia kampeni hiyo itakayodumu kwa kipindi cha miezi miwili.

Bi. Mworia amewasihi wateja wa Vodacom kuendelea kutumia huduma zinazotolewa na kampuni hiyo kama vile kuongeza muda wa maongezi ili kunufaika na kitita hicho cha pesa ambacho kampuni ya Vodacom imepanga kuwazawadia wateja wake.

Tags: