
Uchaguzi mkuu nchini Nigeria unatarajiwa kufanyika tarehe 25 mwezi huu
Shambulio hilo linajiri chini ya mwezi mmoja katika uchaguzi mkuu nchini humo.Polisi katika jimbo la Anambra wamesema watu wenye silaha walivamia ofisi ya Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi (Inec) huko Ojoto mapema Jumatano.
Msemaji wa polisi Tochukwu Ikenga aliwaambia waandishi wa habari kwamba kundi hilo pia lilishambulia kituo cha polisi na jengo la makazi lililoko karibu na eneo hilo.Alisema kijana mmoja aliuawa na mwingine kujeruhiwa na kupelekwa hospitalini.
Ni mfululizo wa mashambulizi dhidi ya ofisi za tume ya uchaguzi katika eneo hilo ambapo kundi linalotaka kujitenga, watu wa asili wa Biafra, linafanya kazi. Mashambulizi yanayolenga ofisi za shirikisho hilo la uchaguzi yameibua maswali kuhusu usalama wa maafisa wa uchaguzi na vifaa wakati wa kuelekea uchaguzi huo.