Jumatano , 18th Dec , 2019

Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, kimewasimamisha masomo baadhi ya viongozi wa Serikali ya wanafunzi wa DARUSO, akiwemo Rais Hamis Musa kwa kukiuka taratibu na sheria za chuo hicho, ikiwa ni siku chache baada ya kuipa Bodi ya Mikopo saa 72 kusikiliza mahitaji yao.

Kibao cha Serikali ya wanafunzi DARUSO

Hatua hiyo ni siku chache baada ya Serikali ya wanafunzi kutoa saa 72, kwa Bod ya Mikopo kujibu madai yao kuhusiana na baadhi ya wanafunzi kukosa stahiki zao za mikopo.

Katikia Barua ambayo imesainiwa na Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. William Anangisye imesema viongozi hao wamekiuka taratibu na sheria za Chuo hicho.

Sasa viongozi hao wanatarajiwa kufikishwa kwenye Kamati ya Nidhamu kwa ajili ya kusikiliza shauri lao.