Mwakilishi mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kilimo na Chakula FAO nchini Siera Leone Dkt. Gabriel Rugalema.
Ushauri huo umeeleza kuwa hatua hiyo itawasadia vijana kujikita katika kilimo hifadhi na ufugaji wa kisasa na kupuguza wimbi la vijana wanaozagaa mijini kutafuta ajira kwenye ofisi za serikali na za binafsi.
Ushauri huo umetolewa na mwakilishi mkazi wa shirika la umoja wa mataifa la kilimo na chakula FAO nchini Siera Leone Dkt. Gabriel Rugalema baada ya kutembelea chuo cha kilimo na mifugo cha Igabilo kilichoko wilayani Muleba mkoani Kagera.
Amesema serikali kupitia wizara zake za kilimo na ushirika, mifugo na maendeleo ya uvuvi inatakiwa kutoa elimu kwa watanzania na kuwahamasisha wajikite zaidi katika ufugaji na kilimo hifadhi.
Nao baadhi ya wanafunzi wanaosoma katika chuo hicho wamesema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali mara baada ya kuhitimu masomo ikiwemo ukosefu wa ajira na mitaji ambayo inaweza kuwasaidia ili waweze kujiajiri wenyewe kupitia taaluma wanayoipata katika vyuo mbalimbali nchini.
Kwa upande wake mkuu wa chuo cha Igabilo, Thomasa Niyegela, amewataka vijana kuacha uvivu pindi wanapohitimu katika vyuo vikuu na badala yake wajitume kupitia ujuzi na taaluma zao ambazo ndio nguzo muhimu katika maisha yao.