Ijumaa , 11th Nov , 2016

Vijana wana nguvu, uwezo wa kubadili mwelekeo wa mabadiliko ya tabia nchi endapo watashirikishwa katika vita hivyo.

Vijana wakiwa katika semina

Kauli hiyo imetolewa na mwakilishi wa Katibu Mkuu kuhusu masuala ya vijana Ahmad Al Hendawi anayehudhuria mkutano unaoendelea wa mabadiliko ya tabia nchi mjini Marakech nchini Morocco.

Mkutano huo leo umejikita kwenye kauli mbiu ya vijana na taifa la kesho kwa nia ya kusistiza mchango wa vijana katika kutimiza malengo ya maendeleo endelevu yaani SDG's lakini pia kuchukua hatua dhidi ya changamoto za mabadiliko ya tabia nchi.

Al Hendawi amesisitiza kwamba ushishirikishwaji huo utaendelea kutoa msukumo na kuchagiza utekelezaji wa mkataba wa Paris na malengo ya maendeleo endelevu.