Mazingira ya Hospitali ya Amana jijini Dar es salaam
Vijana Nchini Tanzania wametakiwa kutumia muda wao kujitolea katika kutoa huduma za afya katika hospitali za umma ikiwa ni pamoja na kufanya usafi hali itakayosaidia kuwafariji wagonjwa walio katika hospitali hizo.
Wito huo umetolewa leo na Afisa Afya wa Hospitali ya Amana jijini Dar es salaam. Ally Kasembe wakati alipowapokea vijana mbalimbali wa jiji la Dar es salaam waliokwenda kujitolea kufanya usafi katika Hospuitali hiyo.
Kasembe amesema vijana ndio kundi kubwa katika jamii endapo watajitoa kwa moyo kusaidia huduma za kijamii ikiwa ni pamoja na kutembelea hospitali pamoja na kufanya usafi kutaamsha ari kwa wengine kuiga mfano.




