VIDEO Adam Malima atishiwa bunduki

Monday , 15th May , 2017

Aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Fedha katika Serikali ya Awamu ya Nne. Adam Malima leo amejikuta katika wakati mgumu baada ya askari wa Jeshi la polisi kumtishia bunduki barabarani, tukio lililotokea Masaki karibu na Double tree Hotel jijini DSM.

Aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Fedha katika Serikali ya Awamu ya Nne. Adam Malima.

Inasemekana majibizano hayo ya risasi yamefanyika baada ya Majembe Auction Mart waliokuwa wameambatana na Polisi walipojaribu kukamata gari lilokuwa limeegeshwa pembeni ya barabara ingawa ndani ya gari hilo kulikuwa na dereva.

Kwa mujibu wa watu waliokuwa eneo la tukio wanasema kuwa gari hiyo iliyokuwa imepaki vibaya ilikuwa ikitumiwa na mtoto wa Malima ambaye alikuwa amekwenda IOM kwa shughuli zake.  

Tazama video hizi kujione zaidi