Jumatano , 1st Jun , 2016

Vikundi vinavyounda Mtandao wa Benki za Maendeleo vijini maarufu kama VICOBA, vimetakiwa kuchangamkia fursa za mikopo ya riba na masharti nafuu inayotolewa na serikali, yenye lengo la kuinua hali ya kiuchumi kwa wananchi na wajasiriamali wadogo.

Muenezi wa VICOBA Kitaifa Bw. Mwaka Mwakyusa amesema kuwa serikali kupitia taasisi za fedha, imetoa mikopo kwa vikundi vya wajasiriamali ili waweze kukuza na kuongeza thamani ya biashara zao, ingawa vikundi vingi vinaonekana kutokuwa na uelewa wa kutosha kuhusu mikopo hiyo.

Aidha, vigezo vya kupata mkopo huo ni kikundi cha watu kuanzia watu 15 na kuendelea ambapo dhamana ya mkopo itawekwa na watu watano wa kikundi chake hamna masharati ya dhamana kubwa ambayo yatamuumiza mkopaji.