
Waziri Mkuu Majaliwa akitembelea maeneo yaliyoathrika na tetemeko la Ardhi Mkoani Kagera.
Elimu hiyo imetolewa na Mjiolojia mwanadamizi toka Wakala wa Jiolojia nchini Tanzania, Gabariel Mbogoni jijini Tanga ambapo amesema kuwa takwimu zinaonesha kuwa majeruhi na vifo vingi kwenye majanga ya matetemeko ya ardhi yanatokana na tahuruki ya raia kukosa utulivu.
Mbogoni amesema kuwa madhara mengi yanayotokea kutokana na matetemeko hutokana na kukosekana kwa teknolojia ambayo inaweza kutabiri utokeaji na ukubwa matetekemo hayo hivyo wananchi wanapaswa kuchukua tahadhari zaidi pindi yakitokea ikiwemo kupata elimu ni jinsi gani ya kujiokoa.
Mjiolojia huyo amesema kati ya mambo ambayo mwananchi anaweza kuokoa na kudhurika na majanga hayo ni pamoja na kujificha chini ya meza zilizo imara au kwenye kona za nyuma na kwa mtu aliyeko nje ya nyumba atulie sehemu ambayo ipo mbali na miti pamoja na majengo marefu.