Jumatano , 9th Sep , 2015

Baadhi ya wanawake wanapatiwa matibabu yakiwemo ya upasuaji katika hospitali ya rufaa ya wazazi Meta jijini Mbeya wanalazimika kutembea kwa miguu umbali mrefu kufuata usafiri wa daladala eneo la Kadege kutokana na kukosekana kwa kituo cha daladala.

Mke wa Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe akiwafariji wagojwa waliolazwa katika wodi ya wazazi katika hospitali ya Rufaa ya Meta

Wakizungumza na East Africa Radio kwa nyakati tofuti wameiomba serikali kuangalia uwezekano wa kuanzisha kituo cha daladala ikiwa ni pamoja na kuzielekeza daladala zinazotoka Mbalizi kukatiza hospitalini hapo ili kuwachukua wagonjwa ambao baadhi yao hawana uwezo wa kukodisha magari.

Mwanafunzi wa shahada ya uuguzi wa masuala ya afya ya uzazi kutoka chuo kikuu cha Dar-es-salaam Esta Macha amesema kuwa mwanamke aliyejifungua kwa kufanyiwa upasuaji anaweza kukutana na hatari pindi anapofanya shughuli ngumu ikiwemo kutembea kabla hajapona vizuri.

Kwa upande wake Afisa Mfawidhi wa mamlaka ya usafiri wa nchi kavu na majini SUMATRA, Denis Daudi amesema kuwa tayari mamlaka hiyo imeanzisha 'route' ya kutoka stendi kuu kupitia meta kuelekea Igawilo isipokuwa mwamko umekuwa mdogo kwa watu kupeleka vyombo vyao kwenye ruti hiyo.