Jumapili , 10th Apr , 2022

Naibu Waziri wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe amesema wamejitahidi kukomesha urasimu na ukiritimba kwenye masuala ya usajili wa biashara ya kufungua kampuni.

Naibu Waziri wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe

Mhe. Exaud Kigahe ameyasema hayo kwenye Kipindi Maalum kilichoruka East Africa TV Jumapili saa 1:00 usiku Aprili 10, 2022.

''Kumekuwa kweli na urasimu na ukiritimba wa njoo kesho katika zoezi la kusajili biashara yako, mtu akitaka anaambiwa hujakamilisha hiki badala ya kuambiwa taarifa zinazohitajika ili amalize ndio maana sasa tumeweka dirisha maalum ili kuondoa hiyo,'' - Naibu Waziri wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe.

Aidha ameongeza kuwa, ''Kurasimisha biashara mtu akifuata utaratibu tumewaambia BRELA isizidi siku 7, lakini kama mtu akiwa na taarifa zote hata siku tatu inatosha kurasimisha biashara au kusajili kampuni''.

Tazama Video hapo chini