Jumatatu , 12th Sep , 2016

Upinzani umeshinda uchaguzi wa bunge katika visiwa vya Shelisheli kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya miongo miwili.

Rais wa Visiwa vya Shelisheli James Michel

Kabla ya kutangazwa matokeo rasmi, Rais wa visiwa hivyo, James Michel, aliahidi kufanya kazi pamoja na bunge jipya lilotegemewa kukipokonya madaraka chama chake tawala.

Muungano wa upinzani wa Seychelles Democratic Alliance (LDS) umeshinda viti 15, huku chama cha People's Party kilichoingia madarakani tokea mwaka 1977, kikiwa kimepata viti kumi vilivyobakia.

Kama kiongozi wa taifa na serikali, Rais Michel atalazimika kuongoza nchi huku chama chake kikiwa na viti vichache bungeni.

Uchaguzi wa Shelisheli iliyo na mkusanyiko wa visiwa 115, ulifanyika kwa siku tatu na kumalizika na matokeo hatimaye kutangazwa .