Jumanne , 16th Feb , 2016

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Ulaya leo wamekubaliana kuchukua hatua dhidi ya Burundi inayokumbwa na ghasia, hivyo kuongeza shinikizo kwa viongozi wa serikali kuutatua mzozo wa kisiasa, baada ya mazungumzo ya amani kukwama.

Waandamanaji wakuwa wamemkamata polisi wa kike na kumburuza nchini Burundi katika Mji Mkuu wa nchi hiyo.

Mawaziri hao wamesema Umoja wa Ulaya, Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa wote wametafuta njia za kupata suluhu ya amani, lakini licha ya juhudi zote hizo za jumuiya ya kimataifa, hali nchini Burundi bado inaendelea kuwa ya mvutano.

Taarifa ya pamoja ya mawaziri hao imeeleza kuwa Burundi iko katika ghasia na vitendo vya ukiukaji wa haki za binaadamu vimekuwa vikiendelea.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, umoja huo utachukua hatua madhubuti kwa mtazamo wa kukosekana ishara za amani, bila ya kutoa maelezo zaidi.