
Kwa mujibu wa ripoti ya UNICEF imebainisha kuwa vijana 26 wanapata maambukizi mapya kila baada ya saa moja na kijana mmoja tu kati ya 10 amepima HIV katika nchi hizo za kusini mwa jangwa la Sahara.
Ripoti hiyo imebainisha kwamba wasichana walioko vijijini ndio waathirika wakubwa, na 7 kati ya 10 ya vijana walio na umri wa miaka 15 mpaka 19 wameathirika.
Vijana wenye virusi vya HIV ndiyo kundi pekee lililoathirika ambalo idadi ya vifo haipungui, na takribani vijana milioni 2 ya vijana wenye umri wa miaka 15 – 19 wanaishi na UKIMWI.
Vijana wengi waliofariki kwa UKIMWI waliambukizwa wakiwa watoto (Mama kwa mtoto)
Vijana wengi ambao hufariki na magonjwa yanayoambatana na UKIMWI hupata maambukizi hayo wakiwa wachanga (maambukizi ya mama kwa mtoto), kipindi ambacho baadhi ya wanawake wajawazito wachache wenye maambukizi wakipata huduma ya kuzuia maambukizi kwa mtoto, ambapo ripoti inasema baadhi ya watoto walisalimika kwenye ukuaji wao, bila kujua hali yao ya kiafya kuhusu HIV.
Mkuu wa mpango wa UKIMWI kutoka UNICEF Craig McClure alipokuwa kwenye mkutano Johanesburg nchini Afrika Kusini ambako ripoti hiyo ilitolewa, na kusema ni muhimu kwa vijana ambao hawana maambukizi kupata elimu ya jinsi ya kuwafanya wabaki hivyo.
“Ni muhimu kwamba vijana ambao wameathirika na HIV wanapata matibabu, huduma na kuungwa mkono, wakati huo huo wale ambao hawajapata maambukizi wapate ujuzi na namna ya kuwasaidia kukaa hivyo hivyo, faida tuliyopata katika kuzuia maambukizi ya mama kwa mtoto yanafaa kupongezwa, na uwekezaji wa haraka unatakiwa ili kuweza kuokoa matibabu ya kuokoa maisha ya watoto na vijana ambao wameathirika”, alisema Craig McClure.
UKIMWI NI ugonjwa wa kwanza kuua Vijana Afrika.
Ripoti inaonyesha nusu ya vijana wenye maambukizi ya HIV wanaishi kwenye nchi sita za afrika, ambazo ni Afrika Kusini, Nigeria, kenya, Msumbiji na Tanzania.
Maambukizi hayo yanaendelea kutokea Uganda, ambapo Papa Francis alikuwa huko mwishoni mwa wiki iliyopita, na ripoti ya hivi karibuni inaonyesha kwamba takriban watu milioni 1.5 wanaishi na HIV.
Wakati akiwa nchini humo Papa Francis alikutana na vijana wanaoishi na virusi katka mji wa Kampala, na kusikia ushuhuda wao ambapo aliwafariji kutokata tamaa, pamoja na magumu wanayoyapitia.