
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Mkurugenzi wa kituo hicho kinachojulikana kama University of Dar es Salaam Gender Centre Dkt. Euginia Kafanabo, amesema hayo wakati wa kongamano la jinsia, lililoandaliwa mahsusi kwa ajili ya kuadhimisha siku kumi na sita za kupinga ukatili wa kijinsia.
Je hali ya ukatili wa kijinsia chuoni hapo ipoje kwa sasa? Naibu Waziri wa Jinsia na Mahitaji Maalumu wa serikali ya wanafunzi chuoni hapo Pauline Sylvester, amesema idadi ya matukio ya ukatili tangu serikali hiyo iingie madarakani imepungua ikilinganishwa na ilivyokuwa kabla