Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Lwenge akizindua rasmi moja ya mradi wa maji
Akizungumza jana Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge amesema tatizo zaidi lilikuwepo kwa jiji la Dar es salaam ambapo kuna watu wengi zaidi walikua wanatumia maji kwa kujiunganishia kwa njia zisizo rasmi.
Mhandisi Lwenge amewataka viongozi wa ngazi zote wawajibike katika utunzanji wa miundo mbinu ya maji ili serikali iweze kusambaza maji kwa urahisi huku akiwataka wananchi kutoa ushirikiano juu ya wale wote wanaohusika na uharibu wa miundo mbinu.
Waziri huyo wa Maji ameongeza kuwa wametengeza utaratibu maalumu kwa wauzaji wa maji kwenye magari ambao wakati mwingine walikuwa wanachanganya maji safi na maji taka katika magari yao na kusambaza kwa ajili ya matumizi ya kawaida kwa wananchi.
Aidha Mhandisi Lwenge amesema wametengenza utaratibu wa kutenga mabonde kwa ajili a uhifadhi wa maji kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji ili kuondoa migogoro ya wakulima kujitengenezea mikondo ya maji katika mashamba yao bila utaratibu na kusababisha migogoro.