Jumatatu , 12th Sep , 2016

Sudan Kusini imesema kuwa inakabiliwa na ukosefu wa fedha kwenye balozi zake ambazo zinakumbwa na ucheleweshaji mishahara pia zinaweza kufungwa kutokana na kutolipa kodi.

Rais wa Sudani Kusini, Salva Kiir

Mwenyekiti wa uhusiano wa kimataifa Philip Thom amesema serikali inafanya juhudi kuokoa wanadiplomasia wake ambao wako kwenye hatari ya kufukuzwa na kufikishwa Mahakamani.

Mwezi Machi Serikali ya Sudan Kusini imesema itapunguza idadi ya wafanyakazi wake wa kibalozi kote duniani ili kukata gharama za uendeshaji balozi hizo.