
Hivi karibuni Rwanda na Uingereza ziliingia makubaliano ya kupokea wahamiaji ambao wanatokea nchini Uingereza na kwamba Rwanda ilikua tayari kuwapokea, lakini mpango huo umekua ukipokea ukosoaji mkali kutoka kwa wabunge wa upinzani nchini Uingereza na viongozi wa dini.
Katika mahubiri yake yake ya Pasaka, Askofu Mkuu wa Canterbury , Justin Welby amesema kuwa Mpango wa serikali ya uingereza wa kuwatuma baadhi ya wahamiaji kutoka Uingereza kwenda Rwanda ni "kinyume na asili ya Mungu ", alisema kuwa ufufuo wa Kristo haukuwa muda wa "kuwapatia wengine majukumu yanayopaswa kufanywa na Uingereza".
Waziri Priti Patel amesema kuwa kilichofanyika ni suluhu ya biashara haramu ya kuuza binadamu na kwamba hakuna taifa lenye utu ambalo linaweza kuvumilia kuona vitendo hivyo.
Waziri huyo wa Uingereza pamoja na waziri wa mambo ya nje wa Rwanda Vincent Biruta, wamesema kuwa mwitiko wa dunia juu ya wahamiaji ulikufa .
Vyama pinzani na makundi mbalimbali ya kusidia jamii zaidi ya 160 yamepinga mpango huo na kuita wa kikatiili na wa aibu na kumtaka Waziri Patel kuusitisha mara moja
Moja ya kigezo ni kuwa Rwanda kushutumiwa kuwa na rekodi isiyoridhisha ya haki za binadamu kufuatia ripoti iliyotolewa mwaka jana na umoja wa mataifa.
Waziri Patel ana mwenzake Biruta wametetea kwamba Rwanda inashikilia nafasi ya kuwa nchi salama zaidi duniani huku tayari ikiwa na wakimbizi takribani 130,000 kutoka nchi mbalimbali duniani.