
Kushoto ni William Ruto na kulia ni Raila Odinga
Bado wawili hao wanakimbizana kwenye matokeo ya tafiti mbalimbali zilifofanyika kwa wananchi ambapo Ruto ameachwa kwa asilimia chache na Odinga, huku asilimia zote zikiwa chini ya 45%.
Takwimu mpya zilizotolewa mapema Jumatatu ya wiki hii zinaonyesha kuwa Muungano wa chama cha Azimio la Umoja cha mgombea Raila Odinga, bado unaongoza kwa kukubalika (japo kwa ushindi mwembamba ) dhidi ya kiongozi wa Kenya Kwanza Alliance, William Ruto.
Odinga anaongoza kwa 42 % wakati Naibu Rais Ruto akiwa nyuma yake kwa 39%.