Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohammed Shein
Akilihutubia baraza la wawakilishi visiwani humo,hii leo Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohammed Shein amesema kuwa watahakikisha wanakuza biashara za ndani kwa kuwajengea uwezo wananchi wa Zanzibar katika uzalishaji.
Dkt. Shein amesema kuwa wamedhamiria kuvuka kiwango cha uuzaji wa bidhaa katika visiwa hivyo ambapo kwa mwaka jana walifanikiwa kuuza shilingi bilioni 2 na milioni miambili na tatu nukta nane huku wakilenga kuuza bidhaa za shilingi trilioni 2 bilioni mbili nukta 8.
Rais Shein ameongeza kuwa ili kuyafikia malengo hayo serikali yake itaendelea kutoa elimu kwa Wafanyabiashara juu ya fursa zilizopo nchini Tanzania ikiwa ni pamoja kuanzisha kituo cha kibiashara cha kimataifa katika eneo la Nyamazi.
Amesema kuwa mipango hiyo inafanywa ili kuhakikisha kwamba Zanzibar inaendelea ikiwa na uwiano wa kiuchumi, kijamii na kimazingira ili kufikia lengo lake la milenia na kuelekea katia malengo mapya ya maendeleo endelevu.