
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli .
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo, ikiwa siku moja tangu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kutoa siku nne kwa wafanyabiashara wa zao hilo, kuzinunua kabla serikali haijafanya maamuzi ya kuzifuta leseni za kununulia korosho kwa wafanyabiashara hao.
Akizungumza na wanajeshi pamoja na Jeshi la Kujenga Taifa nchini ambapo aliambatana na Mkuu wa Majeshi nchini Jenerali Venance Mabeyo amesema “tumejifunza wametupa akili mapema wamechelewa na korosho zetu tutaziuza, na msimamo huu pia utaendelea kwenye mazao mengine kwa wale watakaotaka kuchezea wakulima, lazima tujipange kikamilifu.”
“Waliokuwa wameomba wafanyabiashara kununua korosho walikuwa zaidi ya 37, lakini waliojitokeza walikuwa zaidi 15 kwa hiyo walikuwa na mgomo tu ndiyo maana nilimuagiza Waziri Mkuu, atangaze siku nne mwisho jumatatu saa 10 jioni na kama hakuna atakayejitokeza tutaanzisha operesheni korosho, na tutazinunua zote na tutazisambaza wenyewe.”
Aidha Rais Magufuli amewataka wakulima kuendelea kuwa wavumilivu kwamba serikali waliyoiweka haitawaangusha itaendelea kuwapigania ili kuhakikisha wananufaika kupitia zao lao la korosho.