Jumapili , 18th Apr , 2021

Baraza la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira nchini (NEMC) limesema kuwa kuanzia kesho Jumatatu ya April 19 vifungashio visivyokuwa na ubora ambavyo vimezuiwa kutumika havitakiwi kuonekana sokoni na endapo Mfanyabishara au mteja akimatwa adhabu yake ni faini au kifungo jela.

Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Samuel Gwamaka, kushoto ni mifano ya vifungashio vya plastiki (picha kutoka mtandaoni)

Akizungumza na wanahabari Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Samuel Gwamaka amesema kuwa muda uliotolewa na Baraza umekwisha hivyo kinachoendelea sasa ni utekelezaji kama walivyokubaliana na kwassa tiyarai uelewa juu ya vifungashio visivyokuwa na viwango ni vipi kimeshaeleweka 

"Tunaamini kabisa kwamba kwenye masoko, viwanda hatutegemei kuona kifungashio kisichokuwa na kiwango au anuani ya mtengenezaji, kisochukuwa na ruhusa ya tbs,  kuanzia jumatatu tusione kifungashio kisichokuwa na kiwango elimu tumeiotoa na tunaendelea kuitoa, tarehe 8 amabyo ilikuwa mwisho ishapita sasa lakini tumejaribu kuwa waungwana tunaelimisha watu, kuanzia jumatatu tusikione hata hiki kimoja tukikikuta utachukuliwa hatua kwa mujibu wa kanuni la katazo la mifuko ya plastiki na vifungushio la mwaka 2019" amesema Dkt.Gwamaka

Amesema kuwa vifungashio vipya ni rafiki kwa Mazingira hivyo kwa kuzingatia hilo Watanzania kwa pamoja watayatunza Mazingira na iliviingie sokoni lazima vifungashio visivyokuwa na viwango vitoke sokoni

"Ili vifungashio vilivyokidhi viwango viingie sokoni lazima vifungashio visivyokuwa na viwango vitoke sokoni, sasa wewe ulienavyo wasilisha hivyo vifungashio haraka sana kwenye ofisi za NEMC, ofisi za kata au mtendaji ikifika jumatatu tusione kifungashio kisichokuwa na viwango" amesema Dkt.Gwamaka