Jumatatu , 18th Jul , 2016

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala bora, Bi. Angela Kairuki amesema serikali italipa madeni ya wazabuni na ya watumishi wwa serikali bila matatizo baada ya kuhakikiwa na kijiridhisha.

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala bora, Bi. Angela Kairuki.

Waziri Kairuki ametoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki mkoani Morogoro, wakati akizungumza na watumisshi wa Umma kutoka Sekretarieti ya Mkoa wa Morogoro kwenye ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.

Mhe. Kairuki amesema serikali ya awamu ya Tano itaendelea kulipa madeni ya watumishi na wazabuni lwa uhakiki wa madeni hayo utakapofanyika ili kupata deni halali linalodaiwa na serikali na watumishi halali wanaotakiwa kulipwa.

Hatua hiyo imekua mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro. Dkt. Stephen Kebwe kumfahamisha waziri kuwa mkoa huo unadaiwa madeni yenye kufikias kiasi cha bilioni 1.1 kutoka kwa wazabuni na watumishi.