Akiongea leo jijini Dar es salaam Katibu mkuu wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini TUCTA, Nicholaus Mgaya amesema bado waajiri wengi hawachukui hatua madhubuti za kuzingatia usalama kwa wafanyakazi ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa za ajali zinazotokea.
Naibu waziri wa kazi na ajira nchini Tanzania, Dkt. Makongoro Mahanga amesema katika kuadhimisha siku ya usalama mahala pa kazi April 28 mwaka huu, serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali kupitia Wakala wa Usalama na Afya mahali pa Kazi (OSHA) ingawa hali ya vifo na majeruhi kwa wafanyakazi mahala pa kazi nchini kuwa si ya kuridhisha.