Ijumaa , 29th Jul , 2016

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof Makame Mbarawa, amesema kuwa serikali inataka kuiona kampuni ya TTCL, ikitoa ushindani katika soko la mawasiliano nchini.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof Makame Mbarawa.

Waziri Mbarawa amesema hayo jana, Jijini Dar es Salaam, alipozungumza na wafanyakazi wa kampuni hiyo na kuongeza kuwa serikali imefanya mengi kuiwezesha kuwepo kuendelea kuhudumia Watanzania.

Mhe. Mbarawa amesisitiza kuwa serikali tayari imeshailipa kampuni ya Bharti Airtel shilingi bilioni 14.9 na kuachana rasmi na kampuni hiyo na kuweza kujiendeleza wenyewe.

Aidha Waziri Mbarawa amsema ni lazima kubadilika na kufanya kazi kwa juhudi kubwa ili wananchi waridhike huku akikemea tabia ya vyama vya wafanyakazi kutumia muda mwingi kulumbana na kuendesha migogoro isiyo na tija.