
Trump aliamuru kusitishwa kwa shughuli hiyo jana kufuatia mkutano mkali na Volodymyr Zelensky katika ofisi ya Oval wiki iliyopita.
Jana usiku, wakati wa hotuba yake kwa bunge la Congress, rais huyo wa Marekani alisema Ukraine iko tayari kuanza mazungumzo ya amani na kusoma kwa sauti barua aliyopokea kutoka kwa mwenzake wa Ukraine.
Wakati huo huo, Mkurugenzi wa CIA John Ratcliffe ameonekana kuthibitisha kuwa Marekani imesitisha ushirikiano wa kiintelijensia na Kyiv.
Wakati Marekani, Ukraine na Urusi zote zikionyesha dalili za nia ya kuanza mazungumzo ya amani, diplomasia ya juu ya wiki chache zilizopita inaendelea nyuma ya pazia.
Waziri wa Ulinzi wa Uingereza John Healey yuko njiani kuelekea Washington DC leo kukutana na mwenzake wa Marekani Pete Hegseth siku ya Alhamisi.
Kumaliza vita vya Ukraine itakuwa juu ya ajenda, wakati Uingereza inaendelea kufanya kazi na Ulaya na Marekani kufikia makubaliano ya amani.