Ijumaa , 9th Sep , 2016

Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) kwa kushirikiana na Shirika la Viwango (TBS) na wazalishaji wa bidhaa mbalimbali, watazindua kampeni ya Fahari ya Tanzania yenye lengo la kuhamasisha utengenezaji na uzalishaji wa bidhaa bora.

Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF Dkt. Godfrey Simbeye (kushoto) akiwa na Meneja wa Kampeni hiyo Bw. Emmanuel Nko

Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) kwa kushirikiana na Shirika la Viwango (TBS) pamoja na wazalishaji wa bidhaa mbalimbali, watazindua kampeni ya Fahari ya Tanzania yenye lengo la kuhamasisha utengenezaji na uzalishaji wa bidhaa bora zitakazokidhi viwango na masoko ya kimataifa.

Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF Dkt. Godfrey Simbeye amesema Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan atakuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa kampeni hiyo itakayokwenda sambamba na utoaji tuzo kwa bidhaa 50 bora za Kitanzania kupitia tuzo zijulikanazo kama Top 50 Tanzanian Awards 2016.

Meneja wa Kampeni hiyo Bw. Emmanuel Nko amesema tuzo hizo ni muhimu katika kukuza sekta ya viwanda na utoaji wa huduma nchini na kwamba washindi wamegawanyika katika makundi mbalimbali na kuitaja baadhi ya vigezo kuwa ni mchango wa bidhaa katika utoaji wa ajira, upatikanaji wake, gharama na bei ya bidhaa husika pamoja na kiwango cha malighafi za ndani zilizotumika katika bidhaa hiyo.