Jumamosi , 2nd Aug , 2014

Chama cha wanasheriawa Tanganyika TLS kimesema kuwakitafungua kesi mahakamani kuitaka makama itoe ufafanuzi wautata wakisheria nakikanuni uliogubika mchakato wa Katiba mpya, hadi kusababisha baadhi ya wajumbe kususia Bunge Maalum la Katiba

Jenerali Ulimwengu akitoa mada katika Kongamano hilo

Wakizungumza katika Kongamano la Katiba lililoandaliwa na Chama hicho leo jijini DSM, viongozi wa chama hicho wamesema kuwa wataangalia uwezekano wa kwenda mahakamani ili mahakama itoe tafsiri ya kifungu cha 25 cha sheria ya mabadiliko ya katiba kuhusu mamlaka ya Bunge Maalum.

Pamoja na kutoa ahadi hiyo, chama hicho kimesisitiza kuwa #BungeLaKatiba lina mamlaka ya kuboresha na si kubadilisha misingi ya Rasimu ya Katiba mpya.

Nao baadhi ya wazungumzaji katika kongamano hilo wamesema kuwa njia pekee ya kuukwamua mchakato wa kupata katiba mpya ni kwa wajumbe wa bunge maalum la katiba kufikia maridhiano ya kisiasa ndani ya bunge hilo na siyo nje.

Wazungumzaji wakuu wa Kongamano hilo lililohusu mivutano ya makundi katika mchakato wa katiba mpya walikuwa ni pamoja na Jenerali Ulimwengu ambaye katika maoni yake amewataka wananchi wakubali kuwa wana udhaifu, wawe tayari kuuondoa kwa mazungumzo na kwamba mambo yote lazima yazungumwe katika mchakato wa katiba.

Zifuatazo ni baadhi ya nukuu katika hotubaya Jenerali Ulimwengu:-
"Alipoteuliwa Jaji Warioba kuongoza Tume, watanzania walishangilia lakini hawakujua kuwa ilikuwa ni kiini macho tu"
"Mchakato wa Katiba mpya waliopewa akina jaji Warioba ni Misssion Impossible, nawapa pole sana"
"Kama #BungeLaKatiba lina uwezo wa kubadilisha kila kitu, kulikuwa na haja gani ya tume ya Warioba?
"Ukweli ni kwamba CCM hawataki Katiba mpya na walishasema hivyo" je kauli hii ni Kweli?

Kwa upande wake Profesa Patrice Lumumba kutoka nchini Kenya amesisitza kuwa watanzania lazima wapate katiba mpya inayotokana na mawazo ya wananchi kama ilivyo kwa nchi nyingine za Afrika Mashariki na kuongeza kuwa kazi ya bunge maalum la katiba ni kuboresha katika lugha ya kisheria mapendekezo ya tume ya mabadiliko ya katiba.

Professa Lumumba amesema, na hizi ni baadhi ya Nukuu katika hotuba yake :-
"Hakuna nchi duniani ambayo imewahi kukusanya maoni ya wananchi kama ilivyofanya Tume ya Warioba"
"Inashangaza kuona Tume ya Katiba ilivunjwa kabla mchakato haujamalizika, ilitakiwa ibaki hadi mwisho"
"Kwa utafiti wangu, UKAWA walikuwa na sababu ya msingi na inayoeleweka kujitoa katika #BungeLaKatiba"
"Rais @jmkikwete amekiri kuwa alifanya makosa lakini hawezi kuwapigia magoti kwa sababu ya cheo chake"
"Rais akisema kuwa NILITOA MAONI YANGU anamaanisha kuwa NISAMEHENI, kwa hiyo amekiri kuwa alikosea"
"Watanzania tambueni kuwa yanayopikwa haraka pia huoza haraka"
"Wana CCM watambue kuwa ubabe wa kuwa na wingi wa wanachama hautawafikisha popote, wote ni watanzania"
Kama #BungeLaKatiba litaanza bila UKAWA, ni bora liahirishwe ili kuzuia hatari zaidi"
"Kitendo cha kuwaingiza wanasiasa katika mchakato wa Katiba mlifanya dhambi kubwa sana ya asili"

Kwa upande wake mjumbe wa bunge maalum la katiba Mh David Kafulila ameshauri mchakato wa katiba mpya usitishwe kwanza lakini baadhi ya mambo yafanyiwe mabadiliko ikiwemo sheria ya uchaguzi na tume ya uchaguzi kabla ya kuingia uchaguzi mkuu na baadae zoezi la kuandika katiba mpya lianze upya ili lipate muda wa kutosha.