Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Bw. Hiiti Sillo.
Akizungumza na waandishi wa habari katika mkoa wa Arusha mwakailishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Bi. Charys Ugulumwa, ambaye ni Mkurugenzi wa Huduma za Maabara amesema,tangu kuazishwa kwa opesheni mbalimbali uingizwaji wa bidhaa hizo umeonekana kupungua kutokana na wananchi wengi kuwa na uelewa, huku maombi ya bidhaa tiba katika forodha yamekuwa yakiongezeka.
Hata hivyo kwa upande wao waandishi wa habari wamesema uelewa wananchi juu ya bidhaa duni na bandia bado ni mdogo sana hivyo juhudi za uelimishaji zinapaswa kufanyika ili wananchi waweze kushiriki hususani katika maeneo ya vijijini ili waweze kupiga vita bidhaa zilizopigwa marufuku.
Awali akifungua kongamano hilo Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda, amesema wananchi waongeze juhudu katika kufichua wafanyabishara ambao sio waaminifu wanaosambaza bidhaa ambazo zimepigwa marufuku ili kuepusha madhara mbalimbali yanayotokana na matumizi ikiwemo saratani, uzio, magonjwa ya ngozi ulemavu na hata kifo.