Jumatatu , 7th Sep , 2015

BAADHI ya wajasiriamali mkoani Njombe wamenufaika kwa kuinua uchumi wao na kufanya biashara zao kuwa rahisi baada ya kupitiwa na mradi wa miaka mitatu ya kuondokani umaskini mijini na vijijini kwa kupitia teknolojia.

Kaimu Mkurugenzi wa Costech Dkt. Dugushilu Mafunda

Kauli hiyo imetolewa na wajasiriamali walio kuwa katika mradi wa kuondoka umasikini mjiji na vijijini kupitia mawasiliano (Picture Africa) uliokuwa chini wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) ambao ulifungwana mkuu wa mkoa wa Njombe Dr. Rehema Nchimbi baada ya kudumu kwa miaka mitatu.

Akizungumza katika ufungaji wa mradi huo Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH Dr. Dugushilu Mafunda amesema kuwa hapa nchini hakukuwahi kutokea kwa ushahidi kuwa Tehama inaweza kuinua uchumi wa nchi.

Aidha kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Njombe Dr. Nchimbi amesema kuwa wajasilia mali na jamii kwa ujumla iachane na kutumia simu kwa salam pekee na kuzitumia simu kwa manufaa ya kufanya biashara ili kujenga mahusiano mazuri ya kibiashara na kurahisisha biashara kwa kutumia muda mfupi.