Wajumbe wa Kamati ya Ufundi ya Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam (DAWASA) wakiangalia maungio ya mradi wa bomba jipya.
Hayo yamezungumzwa na Mkurugenzi wa Ufundi kutoka Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) Romanus Mwang'ingo ambapo akizungumzia mradi wa Ruvu Chini amesema, umekamilika kwa asilimia 94 na wakaazi wa maeneo yanayopitiwa na mradi huo wa mtambo wa Bagamoyo, wataanza kupata huduma ya maji safi kwa uhakika kuanzia mwezi Juni mwaka huu.
Aidha ameongeza kuwa kwa wakaazi wanaopitiwa na mradi wa maji wa mtambo wa Ruvu Juu, wataanza kupata huduma ya maji safi kwa uhakika ifikapo mwezi Agosti mwaka huu, baada ya kukamilika kwa matengenezo ya mradi huo kwa asilimia 70,
Bw. Mwang'ingo amesema kuwa mradi wa Ruvu chini unatarajia kutoa lita Milioni 270 za maji, kinyume na sasa ambapo ni lita milioni 182 tu, zinazopatikana.
Pia amesema mradi wa Ruvu Juu unatarajiwa kutoa lita milioni 196 za maji zitasambazwa kwa siku, tofauti na hali ilivyo kwa sasa ambapo kwa siku ni lita Milioni 82 tu, hupatikana.