Mwenyekiti wa Chama cha Wasarishaji nchini (TAT),Bw. Zacharia Hans Poppe
Akizungumza East Africa radio Mwenyekiti wa Chama cha Wasarishaji nchini Bw. Zacharia Hans Poppe amesema kuwa madereva wengine wanaendesha migomo pasipo kufuata utaratibu maalum japo linalopeleka kushindwa kufika suluhu ya utatuzi wa matatizo yao.
Zacharia amesema kuwa wao kama waajiri wanafuata sheria na makubaliano ya ajira kwa mwajiriwa hivyo akiona kama mkataba na mwajiri wake ni bora akamgomea mwajiri wake na si kulazimisha wengine kugoma.
Zacharia amesema wamewashauri madereva hao kefungua vyama vya wafanyakazi ambavyo vitafanya makubaliano na waajiri na ambavyo vitakua na nguvu kisheria kupeleka malalamiko yao juu zaidi ili kutatua changamoto zao.
Aidha Zacharia ameongeza kuwa uwepo wa vyama vingi vya madereva hao vinafanya kushindwa kuwa kiongozi mmoja ambaye anaweza kuwawakilisha katika kuyasema matatizo yao jambo ambalo linafanya biashara hiyo ya usafirishaji kukumbwa na mgogoro wa muda mrefu.