Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumisi na Utawala Bora Mhe. Angelah Kairuki amesema serikali kupitia mpango wa kunusuru kaya maskini nchini TASAF kwa awamu ya kwanza na ya pili imefanikiwa kupunguza asilimia 20 ya kaya maskini nchini.
Waziri huyo pia amesema kuwa kupitia mpango huo wananchi wamenufaika na mpango huo wa serikali wenye lengo lakusaidia wananchi kujipatia vipato vyao wenyewe vya kila siku.
Mhe. Kairuki amesema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na watumishi wa ofisi ya rais wa mfuko wa maendeleo ya jamii ambao unashughulika na kunusuru kaya maskini nchini na kuwataka viongozi ambao wanasimamia mpango huo kuhakikisha wanasimamia kwa kuzingatia maadili ya kazi yanavyotaka kwa ajili ya kunusuru kaya maskini nchini hasa zile zenye mahitaji maalum.
Amesema kupitia miradi hiyo ya kupunguza umaskini nchini ni lazima kwanza serikali itatue matatizo ambayo wananchi bado wanayalalamikia na kuwahamasisha wadau wa maendeleo nchini kuchangia miradi mbalimbali ya maendeleo na kuziwezesha kaya maskini nchini kunufaika na malighafi zilizoko ndani ya nchi na kuwaunganisha na fursa mbalimbali ambazo zitawasaidia kuongeza vipato vyao vya kila siku.





.jpg?itok=5cvL0YaP)