
Rais Samia amesema kuwa kuna baadhi ya watu wanaoamini kuwa kuhesabiwa ni nuksi ambapo amesema Serikali isingependa kusikia kuna asilimia ya watu haikuhesabiwa.
Kauli hiyo ameitoa wakati wa zoezi la uzinduzi wa nembo na tarehe rasmi ya Sensa ya watu na makazi zoezi ambalo limefanyika leo Aprili 8, 2022 visiwani Zanzibar.
Amesema ni muhimu kwa kila mtanzania aliye hai kuhesabiwa ili kurahisisha kazi kwa serikali katika mipango ya maendeleo.
Aidha Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema kufuatia ombi la viongozi wa dini kutaka Sensa ya mwaka huu isifanyike siku za ibada serikali imeamua zoezi hilo litafanyika siku za kazi pekee.