Jumapili , 11th Mei , 2014

Serikali ya Tanzania imeelezea kupokea kwa masikitiko na mshituko mkubwa kifo cha balozi wa Malawi nchini Tanzania Hayati. Mhe. Flossie Gomile Chidyaonga

Aliyekuwa Balozi wa Malawi nchini Tanzania Flossie Gomile Chidyaonga enzi za uhai wake

Serikali ya Tanzania imeelezea kupokea kwa masikitiko na mshituko mkubwa kifo cha balozi wa Malawi nchini Tanzania Hayati. Mhe. Flossie Gomile Chidyaonga kilichotokea tarehe 9 Mei 2014 akiwa njiani kupelekwa hosipitalini Agha Khan jijini Dar es salaam.

Akielezea kifo hicho katibu mkuu wa wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa ndugu John Haule amesema, uchunguzi wa madakatari umeonesha kuwa Balozi Chidyaonga amefariki dunia kutokana na maradhi ya moyo kushindwa kufanya kazi.

Mwili wa marehemu unatarajiwa kuagwa kesho saa Nne Asubuhi katika ukumbi wa mwalimu nyerere jijini Dar es salaam na kisha kusafirishwa kuelekea Blantyre Malawi kwa maziko yatakayofanyika siku ya Jumatano.

Miezi miwili iliyopita KURASA ya EATV ilizungumza na hayati Balozi Flossie na aliahidi kendelea kuishawishi nchi yake kushirikiana vyema na Tanzania.