Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Tanzania yakabidhi misaada Malawi

Jumamosi , 25th Mar , 2023

Balozi wa Tanzania Nchini Malawi Humphrey Polepole ameshiriki katika zoezi la kukabidhi misaada ya Kibinadamu kutoka Tanzania kwa Serikali ya Malawi ili kusaidia wahanga wa Kimbunga Freddy

Balozi amekabidhi misaada hiyo ya kibinadamu inayojumuisha Mablanket, Mahema, Unga wa Mahindi kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi Mhe. Nancy Tembo katika Mji wa   Blantrey Nchini Malawi mapema leo 25/03/2023.
Balozi Polepole alibainisha kuwa  wa watanzania, na watu wa Malawi ni jamii moja, na Nia ni kuendekeza umoja uliojengwa na waasisi wa Nchi zetu.

 "Msaada huu wa kibinadamu  utasaidia, katika jitihada za kurejesha matumaini na ustawi kwa ndugu zetu Wananchi wa Malawi", Alisisitiza Balozi Polepole.

Aliongeza kusema kuwa ana imani na wapiganaji  wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania walioenda  Nchini Malawi  watashirikiana na wenzao Wanajeshi wa Malawi, kuhakikisha kwamba misaada iliyotolewa inawafikia  Wahanga wa Kimbunga Freddy.  

Aidha, Tanzania imetoa madawa ya binadamu, ambayo yataweza kusaidia kwenye maeneo ambayo vituo vya afya vimeathirika. Hizi zote ni jitihada za kusaidia Nchi ya Malawi katika kurejesha huduma za afya.

"Tunamshukuru sana Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa Msaada aliotoa kwa Nchi ya Malawi, kwa uwezeshaji wa fedha na wapiganaji wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (Wahandisi wa Medani) ambao watasaidia katika kurejesha hali ya miundo mbinu Nchini Malawi," alisema Balozi.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya nje wa Nchi ya Malawi Mhe. Nancy Tembo amesema ameshukuru Nchi ya Tanzania kwa Msaada wa kibinadamu iliowapatia, ambao umefika katika wakati muafaka.

“Msaada huu ni muhimu kwetu kwa sababu tunao Wanachi wengi ambao makazi yao yameharibika, na tunahitaji msaada wa kila mtu ili kuhakikisha wahanga wa Kimbunga Freddy wanapatiwa huduma za msingi kwa wakati,” alisema Waziri Nancy

Aliongeza kusema Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wamekuja kutusaidia na wataungana na askari wetu wa Nchini Malawi katika kurudisha miundo mbinu iliyoharibika katika hali ya kawaida.

“Nachukua fursa hii kumshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutusaidia katika wakati ambao tunahitaji msaada sana, janga hili ambalo limeathiri Nchi ya Malawi, limegharimu maisha ya watu, na limeharibu miundo mbinu” alisema Waziri Nancy.

Naye Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulika na Operesheni pamoja na Uratibu wa shughuli za Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Uratibu Luteni Kanali Selestine Masalamado ametoa pole kwa wananchi wa Malawi kwa Maafa ya Kimbunga Freddy.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alielekeza Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Idara ya Maafa kuratibu swala la misaada ya kibinadamu kwa ajili ya Wahanga  wa Kimbunga Freddy Nchini Malawi, ambapo kwa awamu ya kwanza helikopta mbili kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania zilisafiri kuja Malawi kufanya kazi za wokozi,  lakini msaada wa pili ilikuwa ni msaada wa fedha kwa serikali ya Malawi na tatu ni kutoa msaada wa kibinadamu kwa Wahanga wa Kimbunga Freddy

HABARI ZAIDI

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa

Maandamano yetu sio kelele za wahuni - Golugwa

Nyumba ambayo mwili wa mwanaume ulikaa hadi kuharibika

Mke aishi na maiti ya mumewe akiamini atafufuka

Ofisa wa idara ya manunuzi na mikataba akimpatia maelezo mmoja wa wananchi wawaliojitokeza kutembelea banda la GGML katika maonesho ya OSHA na kujifunza namna kuzingatia usalama katika shughuli zao za kila siku.

GGML yaja na teknolojia za kisasa za uokoaji

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Rais Samia asema CDF mwanamke atapatikana 2030

Mratibu wa idara ya dharura (ERT) kutoka GGML, Mohamed Mwaimu akimuonesha mama lishe namna ya kuzima moto wakati inatopokea mtungi wa gesi unapopata hitilafu na kulipuka. Mafunzo hayo yametolewana GGML kwa kushirikiana na OSHA kwa akina mama lishe 50 wa mkoani Arusha.

Mama lishe wafundishwa kulikabili janga la moto