
Baadhi ya mitambo ya kuchakata gesi iliyopo mikoa ya Kusini mwa Tanzania
Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Profesa Adolf Mkenda ambaye amesema kuwa hiyo uwekezaji huo ndiyo utakoifikisha Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati.
Profesa Mkenda amesema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa mashauriano, baina ya ujumbe wa wafanyabiashara kutoka nchini Norway na wenzao wa Tanzania kwa ajili ya kuangalia na hatimaye kuingia mikataba ya uwekezaji wa ubia katika miradi ya uzalishaji wa nishati.
Wizara ya Nishati na Madini imewakilishwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Bi. Juliana Pallangyo ambaye amesema mahitaji ya nishati ya umeme kwa sasa ni megawati 3500 wakati uwezo uliopo ni wa kuzalisha megawati 1500 na kwamba ujio wa wafanyabiashara hao ni muhimu mipango ya maendeleo ya kiuchumi.
Kwa upande wake Balozi wa Norway hapa nchini Bi. Hanne-Marie Kaarstad amesema nchi yake imejipanga kuhakikisha kuwa inaendelea kuwa mbia muhimu wa Tanzania hasa katika eneo la uendelezaji wa nishati, eneo ambalo nchi hiyo ina uzoefu wa muda mrefu.