Ijumaa , 9th Sep , 2016

Kulingana na takwimu ya hali ya chakula na kiwango cha upatikanaji wa mahitaji ya chakula nchini, Tanzania ina kiwango cha utoshelevu wa ziada wa chakula kwa silimia 123 % ambapo nafaka ni asilimia 113% na yasiyo nafaka ni asilimia 140%.

Dkt. Charles Msonde

Akiongea mapema leo Bungeni mjini Dodoma juu ya hali ya uzalishaji wa mazao ya chakula kwa mwaka 2015/2016 na upatikanaji wa chakula kwa mwaka 2016/2017 , Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba amesema tathmini ya awali inaonesha kuwa uzalishaji wa chakula utafikia tani 16,172,841 za chakula, kwa mlinganisho wa nafaka ambapo tani milioni 9 ni za mazao ya nafaka huku tani milioni 6 ni za mazao yasiyo ya nafaka.

Dkt. Tizeba amesema kuwa Ili nchi ijitosheleze kwa mahitaji ya chakula kwa mwaka 2016/2017 Tanzania inahitaji tani milioni 13,159,326, ambapo tani milioni 8 ni mazao ya nafaka na tani milioni 4 ni za mazao yasiyo nafaka.

Aidha amesema kimkoa hali ya chakula kwa mwaka 2016/2017 inaainishwa kuwa ya ziada katika mikoa 11 kwa viwango vya asilimia 122 na 222, huku utoshelevu ukiwa katika mikoa 12 kwa viwango kati ya asilimia 103 na 118 na uhaba katika mikoa 2 kwa viwango vya asilimia 3 na 93 moja wapo ikiwa ni Dar es salaam.

Katika mikoa 15 yenye uhaba zipo halmashauri 43 zenye uhaba mkubwa wa chakula, amesema